Papa Leo XIV afanyiwa apasuliwa mapafu kuondoa saratani
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, amefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Gemelli, jijini Roma ambapo madaktari wamefanikiwa kuondoa kivimbe kidogo kwenye sehemu ya chini ya pafu lake la kulia, Ofisi ya Habari ya Papa mjini Vatican imeeleza.
Kwa mujibu wa vatican, Papa Leo XIV amefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Gemelli alasiri ya Oktoba 13, 2026 jambo ambalo lilipangwa, imeeleza taarifa kutoka kwa Dk. Luigi Carbone na Profesa Stefano Margaritora iliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Baba Mtakatifu.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa maadaktari wa upasuaji wameondoa sehemu ya chini ya pafu la kulia la Papa kivimbe kidogo ikifafanua: “Ili kuhakikisha upasuaji mkali, sehemu ya chini ya pafu la kulia imeondolewa kwa kutumia mbinu ya usaidizi wa video,(video-assisted technique,).”
Taarifa za kitabibu zimeeleza kwamba tishu zilizochunguzwa wakati wa upasuaji zilithibitisha utambuzi uliobainika baada ya vipimo vilivyofanywa awali.
“Uchunguzi wa (histological examination) histolojia ya ndani ya upasuaji imethibitisha utambuzi wa saratani aina ya Adenokarsinoma aliyokuwa nayo Papa Leo XIV, ambayo ni uvimbe mbaya chini ya mapafu, kama ilivyoshukiwa kutokana na uchunguzi wa kabla ya upasuaji,” madaktari wamesema.
Taarifa hiyo ya Vatican imebainisha kwamba Papa alikaa katika chumba cha upasuaji kwa takriban saa tatu, huku upasuaji wenyewe ukichukua takriban dakika 90., huku madaktari wakisema upasuaji huo umefanikiwa na haukuwa na matatizo yoyote.
Habari njema Mapumziko
Hata hivyo habari njema ni kwamba, Papa Leo XIV aliamka vizuri baada ya upasuaji na baada ya muda mfupi wa uangalizi, alirejea chumbani kwake ghorofa ya 10 ya Hospitali ya Gemeli ambapo atalazwa kwa wiki moja. Profesa Margaritora ndiye aliyeongoza timu ya upasuaji, akisaidiwa na Profesa Elisa Meacci, Dk. Maria Teresa Congedo na Dk. Leonardo Petracca Ciavarella.
Taarifa mpya
Habari zaidi zinaeleza kwamba leo, Ofisi ya Habari ya Vatican inatarajiwa kutoa taarifa mpya kuhusu jinsi Papa alivyopitisha usiku na matokeo yoyote ya vipimo yaliyopatikana.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Vatican, Matteo Bruni, baada ya upasuaji, Papa Leo XIV aliomba chakula cha jioni na akatumia muda wa jioni akiwa na makatibu wake pamoja na wafanyakazi wengine wa Vatican.
Mapema jana, iiliripotiwa kuwa Papa Leo XIV anatarajiwa kulazwa Hospitali ya Roma kwa ajili ya kuondolewa uvimbe kwenye mapafu.
Ilielezwa kuwa Papa Leo ameweka hadharani kuhusu tatizo kubwa la kiafya linalomhusu, akifichua ugunduzi wa uvimbe huo mdogo wakati wa sala yake ya Jumapili adhuhuri na kutangaza kwamba anataka uondolewe.
Vatican imesema Papa Leo XIV alitarajiwa kulazwa katika Hospitali ya Gemelli leo Jumanne asubuhi, lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu muda wa upasuaji wenyewe.
Upasuaji huo, ambao kwa kawaida hufanywa mtu akiwa amepigwa ganzi ya jumla (mwili mzima), iwapo Papa Leo atafanyiwa, utamhitaji kukaa hospitalini kwa wiki moja.
Tayari Vatican imefuta mikutano ya hadhara ya Papa siku ya Jumatatu hadi Oktoba 20.
“Haya ni mambo yanayoweza kutibiwa vizuri sana,” amesema Dk. Lorenzo Spaggiari, Mkurugenzi wa Upasuaji wa kifua katika Taasisi ya Ulaya ya Matibabu ya Saratani (EIO), ambaye hata hivyo hahusiki na matibabu ya Papa, lakini anayeifahamu timu ya madaktari ya Hospitali ya Gemelli.
Teknolojia ya roboti kutumika?
Spaggiari alisema anatarajia timu ya madaktari wa Gemelli kufanya uchunguzi wa biopsy ili kubaini kama Leo ana saratani ya mapafu, ikifuatiwa na kuondolewa kwa sehemu ya mapafu iliyo na uvimbe.
Alisema uchunguzi wote unaweza kufanywa kwa kutumia mbinu za roboti, na unaweza kufanywa mfululizo, huku mgonjwa akiwa amepigwa sindano ya ganzi na timu tofauti za wataalamu.
